Thursday, 2 January 2014

Yadaiwa Bwana Karegeya kaaga dunia




kwaheli mwaka 2013 karibi 2014..




Polisi nchini Afrika Kusini wamesema kuwa aliyekuwa mkuu wa idara ya

ujasusi wa Rwanda, Patrick Karegeya, amepatikana ameaga dunia katika hoteli moja mjini Johannesburg.
Bwana Karegeya amekuwa akiishi uhamishoni nchini Afrika Kusini kwa muda wa miaka sita iliyopita.
Karegeya alipokonywa cheo cha kanali baada ya kutofautiana na mshirika wake wa zamani, rais Paul Kagame wa Rwanda, ambaye alimshutumu kwa kuhusika na mashambulio ya kigaidi mjini Kigali.
Katika taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari, na chama cha upinzani cha Rwanda National Congress, RNC, inasema kuwa Karegeya alinyongwa ndani ya chumba chake.
Hata hivyo mamlaka nchini Afrika Kusini haijathibitisha madai hayo.

No comments:

Post a Comment