
MAZINGIRA YETU

![]() |
| Marais |
"LEO NIMEAMKA NIKAWA NA WAZA NANI ATAKUWA RAIS WANGU 2015,JE WEWE MWENZANGU UMESHAMFIKIRIA MTU NISHAWISHI!!!!!"
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, amesema uzee
haupaswi kuwa kigezo cha kumtosa mtu anayetaka kugombea urais 2015, kwa
vile fursa hiyo siyo sawa na kutafuta uzuri ‘urembo’ bali kumtafuta
kiongozi atakayebadilisha nchi irudi kwenye uadilifu ambao umepotea.
“Kuna suala la kutafuta vigezo ambavyo havina maana, wengine
wanazungumzia juu ya ujana na uzee, haya siyo mashindano ya uzuri
tunazungumzia kiongozi wa nchi, katika hali ngumu tuliyokuwa nayo kweli
unaweza kujaribu urais,” alisema.
Sitta alisema hayo jana wakati akihojiwa katika kipindi cha Medani za
Siasa na Uchumi kinachorushwa na kituo cha televisheni cha Star Tv
kuhusu siasa za Tanzania.
Alisema wapo wanaosema umri wa
kugombea urais upunguzwe uwe miaka 30 na kutolea mfano wa nchi kama
Marekani bila kufanya utafiti wa kina katika nchi hiyo.
Sitta
alisema nchi kama Marekani inaweza ikaendelea kwa sababu ina taasisi za
msingi kama sekta binafsi ambazo zinaingizia serikali fedha hivyo katika
nchi hiyo huhitaji rais wa ajabu sababu hata suala la chanjo kwa watoto
serikali haihusiki bali limebaki kuwa la sekta binafsi tofauti na hapa
kwetu.
“Mwelekeo wangu mtu wa chini ya miaka 40 itakuwa ngumu
kuongoza nchi katika hali tulipofikia na kwamba kazi kubwa ni
kubadilisha nchi irudi kwenye uadilifu maana tulishajisahau mno
tukawaacha viongozi wakafanya biashara wakiwa ndani ya madaraka na sasa
ni mabilionea,” alisema.
Sitta ambaye amekuwa akitajwa kuwa
miongoni mwa wanasiasa wanaoutamani urais ifikapo mwaka 2015, alisema
wakati ukifika yeye kama mwanasiasa atapima upepo kama awanie au la.
Akizungumzia vyama vya upinzani, alisema kwa kiasi fulani vinaendelea
kupata nguvu ingawa vingeweza kupata umaarufu zaidi kama vingekuwa
vichache kuliko hivi sasa vilivyo vingi.

FUATA NYAYO...



No comments:
Post a Comment