Wednesday, 8 January 2014

  

 

MWANAUME WAKOLA ANASWA NA

 MANOTI KIBAO FEKI SINGIDA LIVE!!

Singida.

Jeshi la Polisi mkoani Singida linamshikilia mtu moja Toyi Wagela maarufu kama Wakola kwa tuhuma za kupatikana na noti bandia 409 zenye thamani ya zaidi ya sh. 3 Millioni /=.

Kamanda Polisi Mkoa wa Singida Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Geofrey Kamwela amebainisha kuwa mtu huyo ambaye ni mkazi wa mkoani Kigoma, alikamatwa na noti hizo akiwa katika Hotel ya Afro Petrol eneo la Chipondoda mjini Manyoni.

Akizungumza na wandishi wa Habari ofisini kwake jana Kamanda huyo alifafanua kuwa noti hizo ni pamoja na 200 za sh. 10,000/= na 209 za sh. 500/= ambazo zilipatikana baada ya kupekuliwa kutokana na mtu huyo kutoa noti moja y ash. 5,000/= kwa mhudumu huyo wakati alipokuwa anataka kulipia huduma ya chakula alichopata.

“Mtuhumiwa Tayi Wagela ambaye alikuwa mteja aliyekwenda katika hotel hiyo, ndipo aliposhtukiwa na mhudumu huyo na taarifa kupelekwa Kituo cha Polisi cha mjini Manyoni, ambapo askari wa jeshi hilo walikwenda huko na kumnasa akiwa na noti hizo".
Alisema Kamanda Kamwela.

Jeshi hilo linaendelea kumuhoji mtu huyo ili kujua undani wa jambo hilo ikiwa ni pamoja na uchunguzi wa kina katika kubaini mahali zilipotengenezewa, watu wengine walioshiriki katika uhalifu huo wa utengeneza wa fedha bandia, na mtandao mzima unaotumika katika shughuli hiyo isiyo halali.

Kamanda alieleza kuwa mtu huyo atafikishwa mahakamani mara upelelezi utakapokamilika na kuwatahadharisha wananchi kuwa makini na noti za bandia ambazo zinawezi kuwa katika mzunguko wa biashara mbalimbali mkoani Singida pamoja na kutoa taarifa ili hatua za kudhibiti ziweze kuchukuliwa na serikali kwa mujibu wa sheria.


Twiga...utajili wa Tanzania

Tuesday, 7 January 2014

Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini, Zitto Z. Kabwe

ZITTO KABWE ASHINDA HUKUMU YA KESI YAKE

Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe.
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, leo imetoa hukumu ya kesi ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe ambapo imempa kinga ya muda kutojadiliwa uanachama wake na Kamati Kuu ya Chadema!Chanzo:www.globalpublishers.info

Dar es Salaam.Mbunge wa Musoma Vijijini (CCM), Nimrod Mkono ametoa ufafanuzi juu ya uhusiano wake na Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe.
Hatua hiyo ya Mkono imekuja baada ya Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu kumtuhumu kuwa aliwahi kumpa Zitto magari mawili.
Katika taarifa yake aliyoitoa jana, Mkono alisema kuna magari mawili yanayohusishwa na Zitto na kuyataja kuwa ni Toyota Land Cruiser na Nissan Patrol.
“Sijawahi kumpatia Zitto magari, isipokuwa kuhusu hiyo Land Cruiser, nilitoa msaada wa kuwanusuru Zitto na Mbowe (Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe), kule Tarime kwenye msiba wa marehemu Chacha Wangwe (aliyekuwa Makamu Mwenyekiti Chadema), kwani walikuwa wakitishiwa kupigwa.”
Alisema alitoa gari hilo lililokuwa na Bendera ya Bunge liwachukue Mbowe na Zitto na kuwapeleka Mwanza... “Walipofika Mwanza, Zitto aliwasiliana na mimi kuhusu ununuzi wa gari hilo na kupitia wakala wangu nilimuuzia,” alisema Mkono.
Kuhusu Nissan Patrol, Mkono alisema lilikodishwa kwa Zitto na mpaka sasa bado analipa gharama za kulikodisha...
“Hata nyaraka za umiliki wa gari hili ninazo mimi mwenyewe kama mmiliki halali. Ninamiliki magari mengi tu hata wewe mwandishi ukitaka Vogue (aina ya gari) nitakukodisha tu,” alisema Mkono.
Alisema wanafahamiana kwa siku nyingi hata kabla ya Zitto kuwa mbunge na kwamba aliwahi kufanya mazoezi kwa vitendo katika ofisi yake (Mkono), alipokuwa mwanafunzi.

Kuhusu tuhuma kwamba anawahonga wapinzani wake wajitoe katika uchaguzi ili apite bila kupingwa alisema katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2000, 2005 na 2010 alipita bila kupingwa kutokana na uchapakazi wake wa kiwango kikubwa.
Mkono pia alijibu tuhuma zilizotolewa na Zitto jana kwamba Mbowe alipewa mamilioni ya fedha na Mkono kwa nyakati tofauti na kusema hajawahi kutoa fedha zozote kusaidia Chadema.
Zitto akana
Katika hatua nyingine, Zitto ameitaka Chadema kumwandikia mashtaka mapya yaliyoibuliwa na Lissu ili aweze kujitetea.
“Mashtaka yangu ni yale tu ya waraka na kugombea uenyekiti na shtaka moja la masuala ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC). Kwa kuwa hawakuniandikia mashtaka hayo kinachobakia ni majungu tu, masuala ya kuhongwa magari ni tuhuma zinazorudiwarudiwa bila ushahidi wowote,” alisema na kuongeza:
“Mkono ananihonga ili nimpe nini? Yeye mbunge na mimi ni mbunge pia. Hiyo hongo tunabadilishana na nini? Katika kumaliza Shahada yangu ya Uzamili ya Sheria na Biashara nilifanya `internship’ (mafunzo kwa vitendo) kwa Mkono na hivyo kuna uhusiano wa kikazi wa baba na mtoto.”
Zitto alisema kuwa Mkono ni kama mzee wake na suala la kumpa chochote kile si hoja.
Kitila amruka Slaa
Aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Dk Kitila Mkumbo amesema kauli zilizotolewa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Wilbrod Slaa kuwa alikiri kwamba Zitto alikuwa akiujua waraka wa Mkakati wa Mabadiliko 2013, ni za kutunga.
Juzi, wakati akieleza uamuzi wa kikao cha Kamati Kuu kuwafukuza uanachama aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho, Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba na Dk Kitila, Dk Slaa alisema wakati akihojiwa na Kamati Kuu, Dk Kitila alisema Zitto alikuwa akiujua waraka huo.
“Siyo kweli. Hata siku moja sijawahi kukiri kwamba Zitto alikuwa akiufahamu waraka, kilichosemwa na Dk Slaa ni uongo.”
Mwigamba afafanua
Mwigamba alisema hakuhojiwa na Kamati Kuu kwa sababu yeye ni Msabato na Siku ya Sabato, hairuhusiwi kufanya jambo lolote zaidi ya kumwomba Mungu.
“Waliniita Ijumaa (Januari 3) ili nihojiwe lakini mpaka saa 12 jioni sikuwa nimehojiwa na niliwaeleza kuwa jua likizama sitakubali kuhojiwa kwa sababu itakuwa imeanza Siku ya Sabato,” alisema.
Alisema kikao cha Kamati Kuu kiliendelea Januari 4, mwaka huu, pia hakuweza kwenda kuhojiwa kwa sababu ilikuwa Sabato, pia alikuwa kanisani, “Niliwaambia kuwa nipo tayari kuhojiwa Jumapili, hawakunijulisha kama wameridhia.”
Chanzo: mwananchi.co.tz

MWENYEKITI WA CHADEMA TEMEKE AVAMIWA, APIGWA, ATUPWA UNUNIO..!

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wilaya ya Temeke na Mjumbe wa Kamati Kuu ya cha hicho, Joseph Yona akitolewa eneo la tukio. (Picha na Millard Ayo)
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wilaya ya Temeke na Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, Joseph Yona (33), amepigwa na watu wasiojulikana na kisha kutupwa kwenye eneo la Ununio Kawe jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo.
Mashuhuda wa tukio hilo wanadai walisikia kelele za mtu kupigwa saa tisa usiku.
Mwenyekiti huyo anadai alichukuliwa nyumbani kwake Mtoni Kwa Aziz Ally na watu wasiojulikana waliokuwa na gari kama la polisi wakidai wananipelekea kituoni kabla ya kuanza kunishambulia kisha kunitupa.

HEBU CHEKI TASWIRA KUTOKA NJE YA MAHAKAMA KUU DAR KABLA YA HUKUMU YA ZITTO...!

Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini, Zitto Z. Kabwe pamoja na Mwanasheria wake,Albert Msando (kulia) wakiwasili katika Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam leo huku wakiongozana na wafuasi wanaopinga kuvuliwa uongozi wake,tayari kwa kwenda kusikiliza kesi yake aliyoifungua dhidi ya Chama Chake cha CHADEMA inayosikilizwa leo Mahakama Kuu.
Polisi wakiwadhibiti wafuasi wa Zitto na wale wanaompinga nje ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar kabla ya hukumu kutolewa.
Wafuasi wa Zitto wakiwa na mabango.
 
 
Wanaompinga Zitto wakiwa na mabango yao nje ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.
Polisi wakituliza vurugu nje ya Mahakama Kuu leo.
Ulinzi ukiwa umeimarishwa katika mlango wa kuingia Mahakama Kuu leo.
Ulinzi mkali nje ya Viwanja vya Mahakama Kuu.

Royal Free Hospital, Hampstead, London UK.


kilimanjaro




Samuel Kumalija Chagula
Beloved father, grandparent and dear friend to many Samuel Kumalija Chagula, died peacefully aged 63 on Monday 23rd December at 6:20am in the Royal Free Hospital, Hampstead, London UK.

Samuel touched many with his great sense of humour, charm, intelligence and an uncanny ability to brighten any room he walked into. As he often remarked, ‘Life is dynamic’ and it is perhaps this that sums him up best. Fondly remembered, never forgotten, Samuel was a ‘true man of the people’ and will be dearly missed by all that knew him.
Samuel is survived by his mother Asha, children Josephine, James, Gosbert, Henry, Diana, Caroline and grandchildren Dalvin, Denzil, Daniel and Dominic.
If wishing to make a contribution towards funeral costs, please transfer funds into the bank account listed below. Please ensure to that you include your full name when asked for a reference.

Account Holder: Ms Josephine Chagula
Bank: Halifax
Sort code: 11-04-16
Account number: 00232703
Funeral Details 
12pm January 17th 2014
Hendon Cemetery Chapel 
London, Holders Hill Rd, London NW7 1NB
*Funeral to be followed by Reception at ‘The Claddagh’ in Hendon, Church Road, NW4 4EA

For more information please contact one of the family members listed below:
Josephine Chagula: josephinejames04@yahoo.co.uk 
-07941 569 052
James Chagula: jchagula@hotmail.com 
– 07453 816 484
ngorongoro
                       Gosbert Chagula: gosbertc@gmail.com 
– 07779 263 188

Thursday, 2 January 2014

Yadaiwa Bwana Karegeya kaaga dunia




kwaheli mwaka 2013 karibi 2014..




Polisi nchini Afrika Kusini wamesema kuwa aliyekuwa mkuu wa idara ya

ujasusi wa Rwanda, Patrick Karegeya, amepatikana ameaga dunia katika hoteli moja mjini Johannesburg.
Bwana Karegeya amekuwa akiishi uhamishoni nchini Afrika Kusini kwa muda wa miaka sita iliyopita.
Karegeya alipokonywa cheo cha kanali baada ya kutofautiana na mshirika wake wa zamani, rais Paul Kagame wa Rwanda, ambaye alimshutumu kwa kuhusika na mashambulio ya kigaidi mjini Kigali.
Katika taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari, na chama cha upinzani cha Rwanda National Congress, RNC, inasema kuwa Karegeya alinyongwa ndani ya chumba chake.
Hata hivyo mamlaka nchini Afrika Kusini haijathibitisha madai hayo.

Monday, 23 September 2013

SITTA AONGELEA UMRI WA MGOMBEA URAIS 2015



 
 
MAZINGIRA YETU
 
 
Marais
"LEO NIMEAMKA NIKAWA NA WAZA NANI ATAKUWA RAIS WANGU 2015,JE WEWE MWENZANGU UMESHAMFIKIRIA MTU NISHAWISHI!!!!!"
 
 
 
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, amesema uzee haupaswi kuwa kigezo cha kumtosa mtu anayetaka kugombea urais 2015, kwa vile fursa hiyo siyo sawa na kutafuta uzuri ‘urembo’ bali kumtafuta kiongozi atakayebadilisha nchi irudi kwenye uadilifu ambao umepotea.

“Kuna suala la kutafuta vigezo ambavyo havina maana, wengine wanazungumzia juu ya ujana na uzee, haya siyo mashindano ya uzuri tunazungumzia kiongozi wa nchi, katika hali ngumu tuliyokuwa nayo kweli unaweza kujaribu urais,” alisema.
Sitta alisema hayo jana wakati akihojiwa katika kipindi cha Medani za Siasa na Uchumi kinachorushwa na kituo cha televisheni cha Star Tv kuhusu siasa za Tanzania.

Alisema wapo wanaosema umri wa kugombea urais upunguzwe uwe miaka 30 na kutolea mfano wa nchi kama Marekani bila kufanya utafiti wa kina katika nchi hiyo.

Sitta alisema nchi kama Marekani inaweza ikaendelea kwa sababu ina taasisi za msingi kama sekta binafsi ambazo zinaingizia serikali fedha hivyo katika nchi hiyo huhitaji rais wa ajabu sababu hata suala la chanjo kwa watoto serikali haihusiki bali limebaki kuwa la sekta binafsi tofauti na hapa kwetu.

“Mwelekeo wangu mtu wa chini ya miaka 40 itakuwa ngumu kuongoza nchi katika hali tulipofikia na kwamba kazi kubwa ni kubadilisha nchi irudi kwenye uadilifu maana tulishajisahau mno tukawaacha viongozi wakafanya biashara wakiwa ndani ya madaraka na sasa ni mabilionea,” alisema.

Sitta ambaye amekuwa akitajwa kuwa miongoni mwa wanasiasa wanaoutamani urais ifikapo mwaka 2015, alisema wakati ukifika yeye kama mwanasiasa atapima upepo kama awanie au la.

Akizungumzia vyama vya upinzani, alisema kwa kiasi fulani vinaendelea kupata nguvu ingawa vingeweza kupata umaarufu zaidi kama vingekuwa vichache kuliko hivi sasa vilivyo vingi.


FUATA NYAYO...
 
 
 
 
 
 
 

HABALI ZILIZO PATIKA....KENYA








Taarifa kutoka eneo la Westgate zinasema kuwa Vikosi vya Usalama vya Kenya ndivyo vimelipua sehemu ya jengo kujaribu kuingia ndani kabisa ya jengo hilo!

Endelea kupata updates hapa => http://bit.ly/15g45AH      HABALI ZILIZO PATIKANA HIVI PUNDE KUTOKA KATIKA MITANDAO HUMU DUNIANI    INADAIWA YA KUWA......
Taarifa kutoka eneo la Westgate zinasema kuwa Vikosi vya Usalama vya Kenya ndivyo vimelipua sehemu ya jengo kujaribu kuingia ndani kabisa ya jengo hilo!

Endelea kupata updates hapa ......
                       
                          http://bit.ly/15g45AH

Wednesday, 11 September 2013

BARUA TOKA KWA RAIA MWEMA JUU YA MADAWA YA KULEVYA.






Siku nyingi nilikuwa najiuliza hawa Watanzania wenzangu wanapata wapi pesa za kutesa namna hii? Nilikuwa nashangaa nikitoka out usiku nikiwa nimejidundulizia vipesa vya mtoko kwa zaidi ya miezi sita tena kwa kujibana ajabu, cha
                                                       kushangaza naenda kujionea
jinsi watu wanavyojirusha kwa ufahari wa hali ya juu. Matumizi yao ni kufuru, magari waliyopaki nje ya kumbi za starehe ni ya gharama nisiyoweza kuifikiria! Bei ya mavazi waliyovaa ndio usiseme. Nikifikiria elimu ya watoto wangu, uwiii nachanganyikiwa! mbona wa TZ wenzangu wanapeleka watoto wao kwenye mashule ya gharama ambazo mimi niliziona kama kufuru! mmmh kwani hawa wenzangu wanapata wapi hayo manoti yote? mbona mie siyapati? kama ni mshahara huu huu tena kuna wengine nawazidi mshahara, kama ni bajeti; sidhani kuna anayenifikia kwa kujua kubana matumizi. Kama ni biashara ... mmmh sijaona ya kuwafanya watu wawe hivi... sana sana naona mabutiki yanafunguliwa tuuuuuu na hayana wateja... mashoo room yamesambaaa kila kona sioni wanunuzi, labda biashara ya mabar na glossary naweza sema yanalipa. sasa inakuwaje? Loooh nimeanza kufunguka sasa kumbe wengi wao walikuwa wanashiriki kwa namna moja au nyingine kwenye hii biashara ya DAWA! Biashara iliyopandisha maisha ya Watz kuwa ya juu na kutengeneza matabaka maana imetufanya wengine tuonekane kama hatujui kutafuta pesa na hatujui mipango... Looo umefika wakati wao wa kuumbuka sasa.... naanza kuona dalili za kukosekana kwa wateja kwenye mabaa na maclub, magari ya kifahari kupungua barabarani, makanisani, masherehe na sehemu mbalimbali za starehe! mmmmmm naendelea kusikilizia majina yanayotajwa huko kwenye ushiriki wa madawa! mboni mambo!! masikio yanaanza kuwasha maana tutasikia hata tusiyoyatarajia..... WaTz kiboko! hadi mnakodi meli??? du kumbe nchi hii imeshaoza eeeeeeeh! Ona hospitali zinavyojaa waathirika wa madawa, cheki vituoni ujionee mateja yanavyonesa ..... balaa hili.




 






"EEE MUNGU WAUMBUE WOTE NA BIASHARA HII IFE KIFO
 CHA MENDE, WATOTO WETU WAPONE; AMENI "