Siku nyingi nilikuwa najiuliza hawa Watanzania wenzangu wanapata wapi
pesa za kutesa namna hii? Nilikuwa nashangaa nikitoka out usiku nikiwa
nimejidundulizia vipesa vya mtoko kwa zaidi ya miezi sita tena kwa
kujibana ajabu, cha 
jinsi watu wanavyojirusha
kwa ufahari wa hali ya juu. Matumizi yao ni kufuru, magari waliyopaki
nje ya kumbi za starehe ni ya gharama nisiyoweza kuifikiria! Bei ya
mavazi waliyovaa ndio usiseme.
Nikifikiria elimu ya watoto wangu, uwiii nachanganyikiwa! mbona wa TZ
wenzangu wanapeleka watoto wao kwenye mashule ya gharama ambazo mimi
niliziona kama kufuru! mmmh kwani hawa wenzangu wanapata wapi hayo
manoti yote? mbona mie siyapati? kama ni mshahara huu huu tena kuna
wengine nawazidi mshahara, kama ni bajeti; sidhani kuna anayenifikia kwa
kujua kubana matumizi. Kama ni biashara ... mmmh sijaona ya kuwafanya
watu wawe hivi... sana sana naona mabutiki yanafunguliwa tuuuuuu na
hayana wateja... mashoo room yamesambaaa kila kona sioni wanunuzi, labda
biashara ya mabar na glossary naweza sema yanalipa. sasa inakuwaje?
Loooh nimeanza kufunguka sasa kumbe wengi wao walikuwa wanashiriki kwa
namna moja au nyingine kwenye hii biashara ya DAWA!
Biashara iliyopandisha maisha ya Watz kuwa ya juu na kutengeneza
matabaka maana imetufanya wengine tuonekane kama hatujui kutafuta pesa
na hatujui mipango... Looo umefika wakati wao wa kuumbuka sasa....
naanza kuona dalili za kukosekana kwa wateja kwenye mabaa na maclub,
magari ya kifahari kupungua barabarani, makanisani, masherehe na sehemu
mbalimbali za starehe! mmmmmm naendelea kusikilizia majina yanayotajwa
huko kwenye ushiriki wa madawa! mboni mambo!! masikio yanaanza kuwasha
maana tutasikia hata tusiyoyatarajia.....
WaTz kiboko! hadi mnakodi meli??? du kumbe nchi hii imeshaoza eeeeeeeh!
Ona hospitali zinavyojaa waathirika wa madawa, cheki vituoni ujionee
mateja yanavyonesa ..... balaa hili.
"EEE MUNGU WAUMBUE WOTE NA BIASHARA HII IFE KIFO
CHA MENDE, WATOTO WETU
WAPONE; AMENI "




No comments:
Post a Comment