![]() |
| Tembo |
Kagera. Zaidi ya wahamiaji haramu 45,000 wanaosadikiwa kuishi mkoani humo, bado hawajarejea katika mataifa yao katika kutekeleza agizo la Serikali ya Tanzania la kuwataka kuondoka nchini kwa hiari.
![]() |
| wahamiaji... |
Kanali Massawe amesema kufuatia agizo la Serikali
ya Tanzania kutaka wahamiaji hao kuondoka kwa hiari, msako wa kuwaondoa
kwa nguvu utaanza wakati wowote kuanzia sasa kwa kutumia vyombo vya
dola.
Amesema hadi sasa wahamiaji 10,600 ndiyo
wameondoka lakini waliojificha maporini na mifugo yao ni wengi
ukilinganisha na idadi ya waliotambuliwa.
"Hata hivyo amesema, wanawake waliorejea katika
mataifa yao lakini wamezaa watoto na Watanzania hawana budi kurudi
katika vijiji walikokuwa ili waume zao wawatafutie vibali waweze kuishi
kwa mujibu wa sheria."



No comments:
Post a Comment