Wednesday, 4 September 2013

KAGERA BILA WAHAMIAJI HARAMU INAWEZEKANA

 
 
 
Baragumu la Mnyonge
 
Baragumu
Wahamiaji
Pamoja na kwamba mchakato wa kuanza kwa oparesheni ya kuwasaka na kuwatimulia mbali raia wote wa kigeni wanaoishi nchini kinyume cha sheria ukiendelea, Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Kagera, kitengo cha Upelelezi, Doria na Misako kimeanza kuwashughulikia wale wote wanaokwamisha zoezi la wahamiaji hao kurudi katika nchi zao.

Taarifa zilizopatikana katika kitengo hicho zinasema kwamba baadhi ya viongozi wa vitongoji na vijiji wamekuwa wakichukua pesa kwa wahamiaji hao na kuwaahidi 'kuwalinda' wakati wa oparesheni hivyo wahamiaji hao kuamua kuahirisha kurudi nchini kwao, Mkuu wa kitengo hicho ASIS. Mwakibinga amesema tayari baadhi ya viongozi wameshakamatwa na kufikishwa mahakamani kwa kosa la kuwahifadhi wahamiaji haramu na wengine bado wanaendelea kusakwa katika oparesheni maalumu iliyopewa jina la 'KAGERA BILA WAHAMIAJI HARAMU INAWEZEKANA KWA WEWE KUSHIRIKI KIKAMILIFU'
— at Bukoba Town
Jivunie Utalii wa Tanzania
 

No comments:

Post a Comment