![]() |
| Simba |
Tumeona wiki iliyopita hekaheka ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pale muswada wa Mabadiliko ya Sheria ya Katiba, kambi ya upinzani waliposema kwa sauti kubwa wakitetea ushirikishwaji wa wadau hasa kwa upande wa Zanzibar.
kuelezea hisia zao kwamba wadau wa Zanzibar
walikuwa na haki ya kusikilizwa mawazo yao, maana sheria inayokusudiwa
kutungwa inawahusu pia wao.
Ingawaje zimesomwa barua bungeni kwamba Serikali
ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) ilishirikishwa,lakini ushiriki huo ni wa
upande wa Serikali upande wa wadau ambao tumewasikia siku ya Jumamosi
pale katika Hoteli ya Bwawani wakilalamika kutokushirikishwa.
Asasi saba za kiraia hapa Zanzibar zimelalamika
kwamba hazijawahi kupata fursa ya kushirikishwa katika kutoa mawazo juu
ya muswada wa sheria hiyo ambao umepitishwa bungeni wiki iliyopita
ambao ulizusha malalamiko mengi kutoka kwa kambi ya upinzani ndani ya
Bunge.
Taasisi hizo saba ambazo zinaongozwa na Baraza la
Katiba Zanzibar chini ya mwenyekiti wake, Profesa Abdul Sharif zilisema
Bunge halijawatendea haki kwa kunyimwa fursa ya kutoa mawazo yao katika
sheria hiyo.
Asasi hizo saba ziliamua kuitisha mkutano na
waandishi wa habari kueleza masikitiko yao. Almasi Mohammed Ali, Katibu
wa Zanzibar Youth Forum alikuwa wa kwanza kufungua ukumbi kwa kuwaeleza
waandishi wa habari kwamba kushirikishwa SMZ haina maana kwamba wananchi
wameshirikishwa.
“Muswada ule ulipokuja mwanzo, viongozi wa
Serikali waliitwa Bwawani na sisi raia wa kawaida tuliitwa katika skuli
ya Haile Selassie kutoa maoni yetu huu mbona hatujaitwa,” alihoji Katibu
Almasi.
Alisema haoni sababu kwa muswada huu wa sheria hiyo kupewa fursa
Kwa Serikali peke yake na wao kama raia wakaonekana kama hawana maana.
“Walijua fika kwamba Wazanzibari hawawezi kukubali kuwa wachache katika Bunge la Katiba na bara kuwa wengi,” anasema Ali.
Mwenyekiti wa Baraza la Katiba Zanzibar, Profesa
Abdul Sharif anasema kwa mujibu wa sheria ingelikuwa vyema muswada huo
ukaonekana katika magazeti ili wananchi watoe maoni yao.
Haki za kiraia ni moja katika mambo ambayo yamelitiliwa mkazo
katika Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984. Katiba ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania nayo pia imeweka mkazo huo kwa raia.
Uhuru wa kujieleza ni moja ya haki yetu muhimu
sana. Ni haki inayoweka msingi kwa uhuru mwingine na heshima ya binadamu
ambapo haki ya fikra (right to think) siyo tu kuwa inalindwa kwenye
katiba yetu ya sasa, bali hata kwenye mikataba ya Umoja wa Mataifa
(UN)na Umoja wa Afrika (AU).Bila shaka tutofautiane katika mawazo,
lakini naamini utofauti huo hautaweza kuifanya au kuishawishi Serikali
kukataza haki ya fikra kwa kuwa katiba zote mbili zimelinda haki hizo
kama zilivyolindwa na mikataba ya kimataifa.
Tunaambiwa kuwa uhuru wa kujieleza ni moja ya haki
yetu muhimu hivyo, kuwepo kwa fikra tofauti na mitazamo katika jamii ni
sehemu ya kufaidi haki hii ambayo sio hisani kwa raia. Ni haki
inayoweka msingi kwa uhuru mwingine na heshima ya binadamu kwa ujumla
wake.
Tunaambiwa kuwa uhuru wa kujieleza ni moja ya haki
yetu muhimu sana hivyo, kuwepo kwa mawazo tofauti na mitazamo katika
jamii ni sehemu ya kufaidi haki hii ambayo sio hisani kwa raia . Kama
wadau Zanzibar wangeshirikishwa nina hakika kilichotokea bungeni kwa
kambi ya upinzani kutoka nje wasingefanya hivyo.
Wasingefanya hivyo kwa sababu wasingekuwa na hoja
ya kueleza katika suala la ushirikishwaji wa wadau kwa upande wa
Zanzibar na hivyo kusingekuwepo kwa hisia ambazo zilielezwa na wengi.
Inaeleweka na kila mmoja wetu kwamba uhuru wa
mawazo ni haki inayoweka msingi kwa uhuru mwingine na heshima ya
binadamu hapa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ujumla
wake.
Haitawezekana katika jamii wote kuwa na fikra
zinazolingana juu ya jambo fulani na kwa maana hiyo ndio kambi ya
upinzani walipoona kulikuwa na haja wadau wa Zanzibar nao kutoa mawazo
yao ili yaunganishwe pamoja na yale ya wadau wengine.
Ni suala lililo wazi kwamba ustawi wa jamii una
uhusiano mkubwa na masuala ya haki za binadamu na kwa sababu hiyo
ilikuwa ni haki kwa wadau Zanzibar kutoa mawazo yao katika muswada
uliowasilishwa na kupitishwa bungeni. Tunaungana na wabunge waliokosoa
suala hilo kule Dodoma, maana kama ingekuwa kwa upande wa Tanzania Bara
watu hawakushikirishwa ingekuwa ni sawa, lakini huko wadau wamepatiwa
fursa ya kutoa mawazo yao huku hakuna zaidi ya Serikali. Kwa kawaida
mwanadamu kukiri upungufu si kitendo cha kujidhoofisha bali ni kitendo
cha kujiamini na kujiimarisha. Msimamo wa kujikosoa ni msimamo wa
kimapinduzi ambao unazingatia upungufu wa binadamu katika matendo yake
ya kila siku, iwe katika siasa, jamii na katika mambo mengine.
Mambo yalivyoanza hadi yalivyofikia tamati ya kupitishwa kwa Muswada ule kila mmoja anafahamu.




No comments:
Post a Comment