Kiongozi wa chama cha waasi zamani
nchini Burundi Agathon Rwasa
kuonekana hadharani leo baada
ya kipindi cha miaka mitatu
| Add caption |
Wafuasi wa Kiongozi wa kihistoria wa kundi la uasi zamani nchini Burundi
la FNL, Agathon Rwasa, wanataraji kumuona tena hadharani kiongozi wao
leo kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka mitatu baada ya
kukimbilia mafichoni.
Kwa mujibu wa Aime Magera msemaji wa kiongozi huyo wa kundi la uasi
zamani Agathon Rwasa ambaye aliachana na uasi na kujikita katika siasa
na baadaye kurejea katika mafichoni baada ya vurugu zilizoibuka baada ya
uchaguzi wa rais wa mwaka 2010 ataonekana hadharani leo.
Aime Magera amewaambia waandishi wa habari kwamba Agathon Rwasa yupo
jijini Bujumbura tangu kipindi kadhaa na leo anaonekana hadharani mbele
ya halaiki ya wafuasi wa chama chake cha FNL na wageni waalikwa kutoka
jamii ya kimataifa.
Msemaji huyo wa Rwasa amethibitisha kuwa kiongozi huyo anakuja kukusanya
wafuasi wake na kuwaweka pamoja kwa ajili ya kujiandaa na uchaguzi mkuu
ujao wa mwaka 2015 ambapo atawania kiti cha urais.
Juni 2010 Agathon Rwasa alirejea mafichoni kwa kile alichodai anahofia
usalama wake. Hata hivyo mauaji ya hapa na pale yalifuatia kutoroka kwa
kiongozi huyo aliye vikwa lawama na kundi lake kuhusika katika mauaji
hayo.
Serikali ya Burundi ilimchukulia kiongozi huyo kama kiongozi hatari sana
kwa usalama wa taifa hilo na kuanzisha harakati za kumsaka bila
mafaanikio.
Aime Magera amesema kwamba kiongozi huyo wa upinzani aliachana na uasi
na hawezi tena kureja msituni, na kwamba hajawahi kuhamasisha vurugu
kama inavyo daiwa. Ameongeza kwamba jamii ya kimataifa imechangia
pakubwa katika hatuwa hii.
Duru za kidiplomasia zimethibitisha taarifa hii na kuongeza kuwa juhudi
za jamii ya kimataifa zimefaanikisha kumrejesha kiongozi huyo baada ya
kukubali kuwa hatoendelea kuukana utawala uliopo.
Tangu mwaka 2010, Agathon Rwasa alitajwa kukimbilia nchini DRCongo
katika mkoa wa kivu ya kusini, Tanzania na Zambia, lakini msemaji wake
amesema kiongozi huyo hajawahi kutoka katika ardhi ya Burundi, na
alikuwa akijificha miongoni mwa wananchi ambao walimuhudumia kwa kipindi
chote hiki.


No comments:
Post a Comment