MAHAKAMANI
PINDA AWA WAZIRI MKUU WA KWANZA TANZANIA
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimemfungulia mashtaka
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kutokana na kauli yake aliyoitoa bungeni hivi
karibuni kwamba wanaokaidi maagizo ya dola wapigwe.Hii inamfanya
Mheshimiwa Pinda kuwa Waziri Mkuu wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kushitakiwa mahakamani.
Mkurugenzi wa LHRC, Dk Hellen
Kijo Bisimba alifungua mashtaka hayo katika Mahakama Kuu jana akisema
kuwa wanamshtaki Waziri Mkuu kwa maelezo kuwa amekiuka kifungu cha
Katiba Ibara 13 (1). Pinda ametajwa kuwa ni mdaiwa wa kwanza katika kesi
hiyo namba 24.
Mkurugenzi wa
Maboresho na Utetezi wa LHRC, Harold Sungusia alisema jana kwamba,
mwingine aliyeunganishwa katika kesi hiyo ya kikatiba iliyofunguliwa na
LHRC na Chama cha Wanasheria Tanzania (TLS) ni Mwanasheria Mkuu wa
Serikali, Jaji Frederick Werema.
Mjumbe wa Bodi ya LHRC,
Wakili Dk Ringo Tenga alisema katika kesi hiyo wameangalia zaidi sheria
na hasa haki za msingi za binadamu na kwamba kauli hiyo ya Waziri Mkuu
Pinda inahatarisha haki hizo.
Hata hivyo hatua hiyo ya LHRC
imepingwa vikali na Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP), Dk Elieza
Feleshi akisema hakuna uhalali wa mashtaka yoyote dhidi ya kiongozi huyo
sababu kauli ya Pinda kuwa pigeni haikuwa piga ua.
Alisema
katika kesi hiyo, kuna jopo la mawakili wasiopungua 20 na kwamba
wamepata saini za wananchi 2,029 wanaopinga kauli hiyo ya Pinda na
kuunga mkono kufunguliwa kwa kesi hiyo.
(Kwa habari zaidi tembelea : http://www.dar24.com/)
No comments:
Post a Comment