![]() |
| Mbuga za wanyama |
![]() |
| BARAGUMU LA MNYONGE |
RAIS
Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko ya uongozi katika ngazi za juu za
utendaji wa Serikalini kwenye nafasi za makatibu wakuu na naibu makatibu
wakuu katika wizara mbalimbali, ambapo wapo waliohamishwa,
wataopangiwa kazi nyingine na yumo anayestaafu.
Kauli
hiyo ilitolewa leo jioni na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue
wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
“Rais
amefanya mbadiliko haya kwa lengo kuu la kuimarisha utendaji wa kazi za
Serikali katika ngazi hizo za juu,”alisema Balozi Sefue.
Mabadiliko
yaliyofanywa kwa upande wa makatibu wa wakuu ni kama ifuatavyo; Dk.
Florens Turuka amekuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, awali alikuwa
Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Joyce Mapunjo
Katibu Mkuu Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki(awali alikuwa
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda,Biashara na Masoko, Jumanne Sagini
amekuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu- Tawala za Mikoa na Serikali
za Mitaa(TAMISEMI) awali alikuwa Naibu Katibu Ofisi wa Waziri Mkuu –
TAMISEMI.
Wengine
ni Dk. Servacius Likwalile amekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha,awali
alikuwa Naibu Katibu Wizara ya Fedha, Dk. Patrick Makungu amekuwa
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, awali
alikuwa Naibu Katibu Mkuu katika wizara hiyo, Alphayo Kitanda amekuwa
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi ,Nyumba na Maendeleo ya Makazi, awali
alikuwa Naibu Katibu Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI.
Dk.
Shaaban Mwinjaka amekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi,awali alikuwa
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko, Dk.Uledi
Mussa amekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko, awali
alikuwa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Profesa Sifuni
Mchome amekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi,
awali alikuwa Katibu Mtendaji Mkuu wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania.
Wanaofuata
ni Charles Pallangyo amekuwa Katibu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,
awali alikuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri, Anna Maembe amekuwa
Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, awali alikuwa
Naibu Katibu Mkuu wizara hiyo, Sihaba Nkinga amekuwa Katibu Mkuu wa
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, awali alikuwa Naibu
Katibu Mkuu Wizara hiyo na Sophia Kaduma amekuwa Katibu Mkuu Wizara ya
Kilimo, Chakula na Ushirika, awali alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara
hiyo.
![]() |
| BARAGUMU LA MNYONGE |



No comments:
Post a Comment