SERIKALI YAINGILIA SUALA LA AZAM TV
SERIKALI YAINGILIA SUALA
LA AZAM TV

Sakata la Yanga kugomea udhamini wa Azam TV limechukua sura mpya baada
ya Waziri wa Vijana, Habari Utamaduni na Michezo, Dk. Fennela Mukangara
kuomba kukutana pamoja na Yanga, Azam na uongozi wa Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF).
Katika taarifa Iliyotolewa na Naibu Waziri wa
Wizara hiyo, Amos Makala, ni kwamba Waziri Mukangara ameagiza kukutana
na pande zote Agosti 14, kabla ya Ligi Kuu kuanza.

Yanga walipeleka barua ya malalamiko kwa Waziri Mukangara ya kugomea
udhamini wa Azam TV kwa kile walichodai kulazimishwa kukubali mkataba
huo na kwamba hawajakurupuka kufanya uamuzi wao wa kugomea Azam TV kwani
wamefanya uchambuzi wa kina juu ya makubalino ya kibiashara ya Bodi ya
Ligi (TPL) na Azam TV na wametambua hauna masilahi na klabu yao na ndiyo
maana wamegomea mechi zao kurushwa na Azam TV.
Hata hivyo,
katika maelekezo yake Dk Mukangara kwa Naibu wake Makala alisema,
“Nimeongea na wadau wa soka na narejea barua ya Yanga kwa Waziri,
nafikiri kuna haja ya Serikali kuingilia suala hili kwa kukutanisha
pande zote kabla Ligi haijaanza, nakuelekeza kwa maelekezo yangu
uwawandikie ombi la kuwa na kikao cha pamoja kati ya viongozi wa Yanga,
TFF, Bodi ya Ligi na Azam.”
“Kikao kitakuwa Agosti 14 saa tano
kamili tulizungumze suala hili kwa masilahi ya soka la Tanzania na ili
kuwa na uelewa mzuri wa jambo hili nashauri kila upande uwe na
wanasheria wa taasisi zao,” alisema Mukangara na kuagiza hadi kufikia
leo pande zote ziwe zimeshapata barua hizo za wito.
Tayari Yanga wameshaitisha mkutano wa dharura wa wanachama wao Agosti 18 ili kujadili suala zima la udhamini wa Azam TV.
No comments:
Post a Comment