JAMBO BUKOBA
Wapendwa marafiki wa Jambo Bukoba,
Tunafurahi kuwajulisha kuwa jana tumewapokea Luka na Tine kutoka
Ujerumani ambao tutakuwa nao kwa mwaka mmoja. Tunamshukuru Mungu
wamefika salama wakitokea Dar es salaam kwa basi hadi Bukoba.
Tunawakaribisha sana katika kikosi kazi chetu cha Jambo Bukoba.
Ijumaa Gonzaga alikwenda Karagwe kwa ajili ya kuanza shughuli ya ujenzi wa chumba cha darasa Karalo Shule ya
Msingi. Jumatatu hadi ijumaa tutakuwa Muleba kwa ajili ya semina ya
walimu wa michezo. Tutakuwa na mwalimu Sweetbert toka Katebenga shule ya
msingi kama mwezeshaji. Tutatumia muda huo pia kusaini mkataba wetu na
viongozi wa Halmashauri ili kutengeneza madawati sistini ya shule ya
msingi Kishoju.
Siku ya Alhamisi tulikwenda nane nane katika
uwanja wa Kyakailabwa. Huko tulifurahi sana kujumuika na marafiki, kula
na kunywa na kuona mazao mbali mbali ya wakulima.
Tunawatakia wikendi njema.
Ni sisi wana Jambo Bukoba.
JAMBO BUKOBA
Wapendwa marafiki wa Jambo Bukoba,Tunafurahi kuwajulisha kuwa jana tumewapokea Luka na Tine kutoka Ujerumani ambao tutakuwa nao kwa mwaka mmoja. Tunamshukuru Mungu wamefika salama wakitokea Dar es salaam kwa basi hadi Bukoba. Tunawakaribisha sana katika kikosi kazi chetu cha Jambo Bukoba.
Ijumaa Gonzaga alikwenda Karagwe kwa ajili ya kuanza shughuli ya ujenzi wa chumba cha darasa Karalo Shule ya Msingi. Jumatatu hadi ijumaa tutakuwa Muleba kwa ajili ya semina ya walimu wa michezo. Tutakuwa na mwalimu Sweetbert toka Katebenga shule ya msingi kama mwezeshaji. Tutatumia muda huo pia kusaini mkataba wetu na viongozi wa Halmashauri ili kutengeneza madawati sistini ya shule ya msingi Kishoju.
Siku ya Alhamisi tulikwenda nane nane katika uwanja wa Kyakailabwa. Huko tulifurahi sana kujumuika na marafiki, kula na kunywa na kuona mazao mbali mbali ya wakulima.
Tunawatakia wikendi njema.
Ni sisi wana Jambo Bukoba.

No comments:
Post a Comment