MAMA WA KITANZANIA ANG'AAAAAA SADC
MTANZANIA ACHAGULIWA KATIBU

Dr. Stergomena Tax, ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afrika
Mashariki, amechaguliwa kuwa Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo ya
Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) katika uchaguzi uliofanyika jana jijini
Lilongwe Malawi katika mkutano wa Jumuiya hiyo.
Ktika uchaguzi
huo, Dr. Tax ambaye anakuwa mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo,
alipata asilimia 79 ya kura zote na kumshinda mpinzani wake Bwana Peter
Sinon ambaye ni Waziri wa Uwekezaji, Rasilimali na Viwanda wa
Shelisheli. Hapo awali wadhifa huo ulikuwa unashikiliwa na Dk. Tomaz
Saloma wa Msumbiji ambaye alishinka nafasi hiyo kwa miaka minane, ambayo
ni vipindi viwili mfululizo.
No comments:
Post a Comment