MSAFARA WA MBIO ZA
MWENGE WAPATA AJALI
Magari matano yaliyokuwa katika msafara wa kukimbiza Mwenge wa Uhuru
yalipata ajali jana katika kijiji cha Fufu kilichoko wilayani Chamwino.
Magari hayo yalikuwa yakitokea Wilaya ya Dodoma kuelekea kwenye
makabidhiano wilaya ya Mpwapwa.
Katika ajali hiyo watu tisa
wakiwemo kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru, Juma Ally (32)
wamejeruhiwa na kulazwa katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma. KWa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya
Dodoma ni kwamba hali za majeruhi zinaendelea vizuri.
Ajali hiyo ilisababishwa dereva wa moja kati ya magari ya msafara ,
kushika breki ghafla baada ya kukutana na tuta na kusababisha magari
yaliyokuwa nyuma yake kugonga gari la mbele yake. KWa kiasi kikubwa hali
hii ilisababishwa na vumbi kubwa lililotokana na ujenzi unaoendelea wa
barabara ya kutoka Dodoma – Iringa.
![]() |



No comments:
Post a Comment