Wednesday, 7 August 2013

UWANJA WA NDEGE WA JOMO KENYATTA WAUNGUA

Uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta International uliopo Nairobi Kenya umefungwa kufuatia kutokea kwa moto mkubwa uliotokea mapema leo. 

Kufuatia kufungwa kwa uwanja huo ambao ni mkubwa katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati ambapo unahudumia zaidi ya abiria 16,000 kwa siku, ni ndege za dharura tu zinazoruhusiwa kutua. 

Moto huo ulitokea alfajiri saa 11:00 uliweza kuzimwa hata hivyo taarifa za usalama zimesema kuwa uwanja utaendelea kufungwa ambapo ndege zilizokuwa zitue uwanjani hapo zinaelekezwa kwenye viwanja vingine vikiwemo vile vya Mombasa, Entebbe International Airport - Uganda na Kigali International Airport – Rwanda. 

Bado uchunguzi unaendelea ili kubaini chanzo cha moto huo na pia kuhakikisha kuwa usalama wa abiria na mali unakuwa wa uhakika kabla uwanja haujafunguliwa tena.
Uwanja waungua
 
UWANJA WA NDEGE WA JOMO
 KENYATTA WAUNGUA
 
Ninoma na ninoma
 
No comments:

Post a Comment