Saturday, 17 August 2013

TUONGEE TUELEWANE...

 
 
TUONGEE TUELEWANE...
 Ninaamini watanzania watafaidika zaidi na matumizi mazuri ya mawasiliano
Ninaamini pia matumizi mabaya ya mawasiliano, ikiwemo mitandao ya kijamii sio tija. Tutumie mawasiliano vizuri. Tutumie mitandao ya kijamii kwa maendeleo. Ukipokea ujumbe wa chuki, matusi, uchochezi, udhalilishaji wa mwanamke, mtoto au mwanaume,  
FUTA DELETE KABISA.
  au ignore/puuzia, 
usisambaze kwa wengine.

Tushiriki majadiliano kwa nia njema, tusitukanane, tujibizane hoja kwa hoja, matusi sio sehemu ya hoja. Admin tusimamie vizuri majadiliano ili kuboresha matumizi mazuri. Tusiingilie uhuru wa watu kujieleza, tuutumie uhuru kutoa maoni yetu kwa uhuru tukizingatia uhuru wetu unakutana na uhuru wa wajihi wa wengine!
 

No comments:

Post a Comment