RAIA WA UINGEREZA ASHIKILIWA KWA UJANGILI
RAIA WA UINGEREZA

Jeshi la Polisi nchini linamshikilia raia wa Uingereza kwa tuhuma za
kukutwa na nyara mbalimbali za Serikali zenye thamani ya zaidi ya Sh100
milioni, vikiwamo vipande vinane vya meno ya tembo.
Kwa mujibu
wa taarifa zilizotolewa na Kamanda wa Polisi Kanda MAalumu ya Dar es
Salaam, Suleiman Kova ni kuwa mtuhumiwa huyo ambaye ni Mkurugenzi wa
Kampuni ya Usafirishaji Mizigo (TALL), alikamatwa juzi saa 2:00 usiku
maeneo ya Mbezi Beach, wilayani Kinondoni.
Afande Kova alipopekuliwa nyumbani kwake alikutwa na meno 20 na kucha
22 za Simba, shanga mbalimbali zilizotengenezwa kwa meno ya tembo,
Kasuku na nyara nyingine ambazo hairuhusiwi kumiliki bila kibali.
Alisema uzito wa nyara hizo ni kilo 25, walimkuta na mawe mbalimbali
yanayodhaniwa ni madini sambamba na ganda moja la bomu lenye ukubwa mita
130.
No comments:
Post a Comment