 |
| BARAGUMU LA MNYONGE |
Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Kagera imeanza kampeni ya kuwahamasisha
wahamiaji haramu ambapo mpaka sasa hawajaondoka nchini kurudi makwao
kuomdoka mara moja kabla ya kuanza kwa zoezi la kuwaondoa kwa nguvu
katika oparesheni inayotarajiwa kuanza wakati wowote kuanzia sasa.
Mfawidhi wa kitengo cha Upelelezi, Doria na Misako katika idara hiyo
mkoa wa Kagera ASIS. Jeremiah Mwakibinga
 |
| Mmoja wa Maofisa uhamiaji
akifuatilia kwa makini maelezo yaliyokuwa yakitolewa na ASIS. Mwakibinga
wakati akiongea na viongozi na wananchi wa kijiji cha Ruhama |
alisema kwamba kwa kuanza
kampeni hiyo imeanza katika wilaya ya Bukoba Vijijini na baadaye
itaendelea kwa wilaya zote za mkoa wa Kagera.
 |
| ASIS. Mwakibinga, ambaye ni Mkuu
wa Kitengo cha Upelelezi Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Kagera akisikiliza
swali kutoka kwa mmoja wa wananchi katika kijiji cha Ruhama alipokwenda
kuhamasisha wananchi na viongozi kushirikiana na Idara hiyo kuwataka
wahamiaji haramu kuondoka nchini kwa hiyari |
|
Alisema kwamba kampeni hiyo imelenga si kwa wahamiaji pekee bali pia kwa
viongozi na wananchi kwa ujumla. ''Tunajua kwamba Wahamiaji Haramu
wakituona wanakimbia, mfano tulipofika katika kijiji cha Kagarama, hivyo
kampeni hii tunaifanya kwa viongozi wa vijiji na wananchi pia.
Tumeongea na wananchi
 |
| Kikosi cha Upelelezi chini ya Kamanda Mwakibinga wakiongea na Afisa Mtendaji wa kijiji cha Katerero |
katika vijiji vya Kibirizi, Rugazi, Kagarama,
Masheshe na Katoro kwamba wao washirikiane nasi kwa kuwakataa wahamiaji
haramu kwani wanajua na wanaishi nao siku zote, kuwakataa manake
kuwaeleza ukweli kwamba warudi kwao, pia wananchi wawashinikize viongozi
wao kuwaondoa wahamiaji haramu. Kwa upande wa viongozi wa vijiji na
kata, tumewasisitiza kwamba wafanye juhudi katika kuwahimiza wahamiaji
hawa waondoke, na kama mtu kaambiwa aondoke halafu amekataa basi walete
taarifa ofisini kwetu siye tutamshughulikia.'' Alieleza Mwakibinga.
Wahamiaji haramu kutoka nchi za Rwanda, Burundi na Uganda ambao wapo
katika mkoa wa Kagera inasemekana waliondoka na sasa wameanza kurejea
tena nchini baada ya kuona kuwa Oparesheni aliyosema Raisi wa Jamhuri wa
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dokta Jakaya Mrisho Kikwete ya
 |
| Maafisa Uhamiaji wakiranda mitaani katika kijiji cha Masheshe wilaya ya Bukoba Vijijini |

kuwaondoa kwa nguvu wahamiaji haramu baada ya wiki mbili haifanyiki,
wengi wamerudi wakidai ile ilikuwa ni 'danganya toto' tu hakuna
oparesheni itakayokuja.
 |
| Wananchi wa kijiji cha Kibirizi
wakimsikiliza Kamanda wa Upelelezi Uhamiaji mkoa Kagera wakati alipokuwa
akiongea nao kuhusu suala la wahamiaji haramu mkoa wa Kagera |

No comments:
Post a Comment