Wednesday, 7 August 2013

MKURUGENZI wa Mashitaka nchini (DPP)

 ALIYETUHUMIWA KUMTEKA NA KUMTESA DR.
 
ALIYETUHUMIWA KUMTEKA NA KUMTESA DR. STEVEN ULIMBOKA AFUTIWA MASHTAKA

MKURUGENZI wa Mashitaka nchini (DPP), Dk. Eliezer Feleshi, amefuta kesi ya kuteka na kujaribu kumuua Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari nchini, Dk. Steven Ulimboka, iliyokuwa ikimkabili raia wa Kenya, Joshua Mulundi, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam.

Hati hiyo ya DPP iliwasilishwa mbele ya Hakimu Mkazi Waliarwande Lema chini ya kifungu cha 91(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2002 kwa niaba yake na Wakili Mwandamizi wa Serikali, Tumaini Kweka.

Hatua hiyo imeelezwa kuwa ni baada ya DPP kuona hana haja ya kuendelea kumshitaki kwa makosa hayo ambayo yalikuwa hayana dhamana.

Hakimu Lema alikubaliana na hoja hiyo na akamfutia kesi hiyo Mulundi ambaye yupo gerezani tangu Julai 13, mwaka jana.
Hata hivyo muda mfupi baada ya Hakimu Lema kumfutia kesi hiyo Mulundi, askari kanzu walimkamata tena na kumfikisha kwa Hakimu Mkazi, Alocye Katemana na kisha Wakili Kweka akaiambia mahakama kuwa upande wa Jamhuri umemfungulia kesi mpya ambayo itakuwa na shitaka moja tu.

Mbele ya Hakimu Katema, wakili huyo alidai kuwa Julai 3, mwaka jana, Mulundi katika Kituo cha Polisi Oystebay alitoa taarifa za uongo kwa ofisa wa polisi kuwa yeye na wenzake walikodiwa kwenda kumteka na kumjeruhi Dk. Ulimboka, jambo ambalo si kweli.

Alidai kosa hilo ni kinyume cha kifungu cha 122 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2002 na kuongeza kuwa upelelezi wa kesi hiyo mpya umekamilika.

PICHANI : Siku Kamanda Selemani Kova alipokuwa anatangaza kuhusu kukamatwa kwa mtuhumiwa mwenye asili ya Kenya kuwa alihusika katika kumteka na kumtesa Dr. Steven Ulimboka.
 STEVEN ULIMBOKA AFUTIWA MASHTAKA

No comments:

Post a Comment