SERIKALI YATOA IDADI YA WAHAMIAJI HARAMU
 |
| Kilimanjaro |
SERIKALI YATOA IDADI YA WAHAMIAJI
HARAMU WALIOKWISHAONDOKA
 |
| Wahamiaji haramu |
 |
| Mali zao |
SERIKALI imesema kwamba operesheni ya kuwaondoa wahamiaji haramu katika
Kanda ya Ziwa itaanza kwa ghafla, huku ikiendelea kusisitiza kwamba
watu wanoaishi nchini bila taratibu za kisheria kuondoka kwa hiari na
mali zao.
Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri wa Mambo ya Ndani
ya Nchi, Dkt. Emmanuel Nchimbi wakati akizungumza na waandishi wa
habari kuhusu wahamiaji haramu waliorejea kwao baada ya agizo la Rais
Jakaya Kiwete alilolitoa Julai 29, mwaka huu katika ziara yake ya mkoa
wa Kagera.
“Nimeshapewa
maelekezo rasmi na Rais Jakaya Kikwete ya kuwaondoa wahamiaji haramu
nitakapoona inafaa. Operesheni itaanza ghafla haiko mbali. Muda mwuafaka
wa kutekeleza vyombo vya dola vitasema. Tunatoa wito waondoke wenyewe
na mali zao bila kunyang’nywa. Wenye mali nyingi wanatakiwa kutoa
taarifa katika vituo vya polisi ili waweze kusindikizwa. Hatutawavumilia wahamiaji haramu,” alisema Waziri Nchimbi.
Aliongeza kuwa wahamiaji hao wanaotaka kuishi nchini wanatakiwa kurudi
nchini kwao kwanza na kufuata taratibu za kisheria kama ambavyo nchi
nyingine zinavyofanya mtu akitaka kuishi nchi yoyote anatakiwa kufuata
taratibu hizo.
Waziri alitoa onyo kwa viongozi wa vijiji
wanaoshirikiana na wahamiaji hao kuwatunza na kusema jambo hilo ni
makosa kisheria , hivyo watakaobainika watachukuliwa hatua za kisheria.
Akizungumzia kuhusu takwimu za wahamiaji hao waliorejea nchini kwao
mpaka sasa ni 10,672 kati ya hao Wanyarwanda ni 6,088, Warundi 4000 na
Waganda 269 ambao wametoka mkoa wa Kagera. Kwa wa mkoa wa Kigoma ni
Warundi 142, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo nane na katika mkoa wa
Geita Wanyarwanda 126 na Warundi 39.
Hata hivyo Waziri
Nchimbi alisema kuna wahamiaji 14 wamerejea nchini tena baada ya
kurudi makwao na kuwataka wasilione jambo hilo kuwa ni mzaha.
Aidha Waziri Nchimbi alisema Serikali ya Tanzania inashukuru ushirikiano
unaotolewa na nchi wanazotoka wahamiaji hao kwa kuwapokea vizuri.
Alifafanua kuwa suala la kuwarudisha wahamiaji hao si la mara ya
kwanza, lilishawahi kutokea. Huku akisisitiza kwamba tatizo linatokana
na sababu mipaka yetu mikubwa na kuna watu wasio wazalendo ambao
wanawapokea na kuwakaribisha kwa kupatiwa zawadi. Hivyo Serikali
inalifanyia kazi jambo hilo.
No comments:
Post a Comment